Cyril na Bob Junior wamaliza beef yao, wafanya collabo

Rapper Cyrill aka Kamikaze na rais wa Masharobaro wameamua kumaliza tofauti zao na kufanya wimbo pamoja.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Cyril kupitia Facebook na kwamba leo ataitambulisha ngoma hiyo.

“Baada ya malumbano yetu kwa kipindi kadhaa baina yangu na Bob Juniour,tumekaa chini nakumaliza tofauti zetu nakuamua kufanya wimbo wa pamoja..kamikaze ft bob juniour ..sikiliza XXL ya clouds fm na BDOZEN leo ntakua na Bob juniour kwenye XCLUSIVE INTERVIEW na pia kuintroduce hio ngoma..dnt miss this!#teamkamikaze #team WW.”