CONFIRMED! Timbaland & Missy Elliott watashiriki kuandaa albam mpya ya Aaliyah

 

Ni official sasa kwamba Timbaland na Missy Elliott watashiriki kwenye maandalizi ya albam ya Aaliyah.

Katika mahojiano mahsusi na Billboard Biz, binamu yake na Aaliyah Jomo Hankerson, ambaye ni mtoto wa mjomba wake na Aaliyah na mmiliki wa Blackground Records Barry Hankerson, amethibitisha kuwa waliokuwa marafiki zake wa karibu na Aaliyah Timbaland na Missy Elliott, watasikika pia kwenye albam hiyo.

"Naweza kukuambia kuwa Timbaland atahusika sana kwenye albam, Missy atahusika sana. Moja ya ngoma ambayo tulikuwa nayo na haikutoka ilikuwa ya Missy ambayo tutairudia.

Hankerson alieleza pia kwanini waliamua kuwajumuisha Drake na rafiki yake /producer Noah "40" Shebib.

"Tuliona kama ni muda sasa. Kuna kizazi kipya ambacho hakimjui kihivyo, na tulitaka kuendeleza muziki wake kwa kizazi kipya.

Hiyo ni miongoni mwa sababu tulitaka kufanya muziki wa kisasa zaidi. Idea ilikuwa ni kuutambulisha tena muziki wake kwa kizazi kipya ambacho hakijui influence aliyotoa kwa muziki wanaousikiliza leo."

Hankerson alisema pia kuwa baba yake Barry Hankerson atahusika katika utayarishaji wa albam hiyo na Drake atasikika kwenye nyimbo nyingi huku 40 akihusika kama producer mwenza zaidi.