
Busta Rhymes atoa albam yake mpya bure
Mwaka huu Busta Rhymes amekuja kivingine baada ya kuamua kutoa albam yake mpya " Year of the Dragon" bure.
Busta aliingia makubaliano na kampuni ya Google August 2011 kabla hata hajasaini na Cash Money kuachia albam hiyo yenye nyimbo 13 ‘exclusively , kupitia huduma ya Google Play Aug. 21.
Kampuni ya Google iliona Busta ni msanii mzuri kuingia kwenye huduma hiyo katika jitihada za kuhusika kwenye burudani pia.
Huduma hiyo ilikuwa ikijulikana zamani kama Android Market tangu kuanzishiwa kwake mwaka 2008, lakini Google iliizindua tena huduma hiyo ya muziki March 6, 2012, kama Google Play.
Ikifanya kazi si kama tu iTunes na Amazon, Google Play inajitahidi kuwapa wasanii umiliki wa kazi zao za sanaa na fursa ya kusambaza kwa wasikilizaji kwa njia nyingi.
Busta na uongozi wake utaendelea kushikirikiana na Google Play ambapo wataweka nguvu zao pia kumsaidia kwenye promotion na performance zingine.
Mpaka sasa Busta ameshauza albam milioni 7.8 kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.