Broke: Mali za Young Buck kupigwa mnada mwezi huu

 

Mashabiki wa Rap nchini Marekani wana matumaini ya kumiliki baadhi ya mali za rapper wa zamani wa kundi la G-Unit, Young Buck kwakuwa baadaye mwezi huu vitapigwa mnada na mamlaka ya mapato nchi Marekani IRS (Internal Revenue Service).

Mamlaka hiyo itauza mali hiyo huko Nashville na vitu vitakavyouzwa vitaoneshwa  July 25.

Rapper huyo anadaiwa karibu dola milioni 11.5 ambazo ameshindwa kurejesha.

Mwezi  April, bosi wa zamani Buck, 50 Cent alijaribu kuzuia kuuzwa baadhi ya vitu ili kuchukua mali anayoimiliki yeye.