Breaking News: Jackson (TPF5) wa Rwanda asainishwa na Universal Music Group

 

Mshindi wa tatu wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa tano Jackson Kalimba amesainishwa mkataba na label Universal Music Group.

Mwimbaji huyo wa Rwanda amekula shavu hilo siku moja tu baada ya Ruth kutajwa kuwa mshindi wa shindano hilo.

Kwa sasa tofauti iliyopo kati ya Jackson na Ruth ni shilingi milioni tano tu za Kenya.

Haijajulikana kama naye anapata pia deal nyingine ya Kshs. 10,000,000 kama Ruth.

Watu wengi walilaani ushindi wa Ruth kutokana na kuwa na uwezo mdogo kiuimbaji ukimlinganisha na Jackson.