Bobby Brown ahukumiwa kwenda jela kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa

Bobby Brown amehuhumiwa kifungo cha siku 55 jela.

Staa huyo mwenye miaka  44 alipatakina kwa kosa la kuendesha akiwa amelewa (DUI)  na pia kwa kuendesha ilhali leseni yake imeshikiliwa na sasa atakaa jela kwa karibu miezi miwili.

Kwa mujibu wa E! News, Bobby – ambaye hakuwepo mahakamani jijini Los Angeles jana (26.02.13) na kuwakilishwa na wakili wake Tiffany Feder – ataripoti jela March 20.

Mwaka jana kama sehemu ya kusamehewa kosa la kwanza alipokamatwa akiwa amelewa Bobby alikubali kwenda rehab.