BBA: Prezzo aangua kilo wakati wa Diary session

Mfalme wa Bling aka Masai Warrior, Prezzo wa Kenya leo amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo wakati wa diary session na Biggie.

“Nina hasira nyingi moyoni mwangu,” alisema Prezzo aliyekuwa akitetemeka huku akijaribu kuzuia machozi yasitoke.

Tangu washiriki hao wagawanywe sehemu mbili,  Upville na Downville, kumekuwepo na mgawanyiko baina yao.

Utofauti huu umekuja kujenga mgawanyiko kati ya Downvillers wa zamani waliojiunga na original Upvillers.

 

Na leo Prezzo amejikuta akishindwa kuzuia hasira zake. Rapper huyo amemwambia Biggie kuwa amejizuia mno kutogombana na baadhi ya washiriki wanaonesha dharau kwake na mpenzi wake Goldie.

Hata hivyo Big Brother amemtaka mkenya huyo kuendelea kujizuia kwasababu vitendo vya ugomvi havivumiliki mjengoni humo.

Ugomvi mkubwa uliopo sasa ni kati ya Keagan wa Afrika Kusini na  Prezzo.