Baada ya kuipiga chini harusi: Game awapiga biti wanaomdharau mpenzi wake

 

Pamoja na The game kuahirisha harusi yake na aliyekuwa mpenzi wake katika mazingira yasioeleweka, rapper huyo ametoa onyo kwa wanaolichukulia tukio hilo kwa dharau.

Juzi ijumaa Game alitumia mtandao wa Twitter kupiga mkwara huo na kumkingia kifua mpenzi wake wa zamani Tiffany Cambridge.

"Kama ndo nyie blogs mnadhani niliahirisha harusi yangu kwa mambo ya kijinga, sikufanya hivyo, aliiamua kufanya hivyo kwa uongo wangu, kumsaliti na kutokuwepo naye vya kutosha, alitweet.

"Mtu mwingine kwenye burudani atakayesema ama kuandika mambo ya kipuuzi dhidi ya mama wa watoto wangu wawili wadogo.. Ntamshtaki.

Game aliamua kuipiga chini harusi hiyo siku chache zilizopita licha ya kujiandaa kwa miezi.

Adui yake mkubwa ambaye Game alimtwanga vilivyo kwenye tukio lililochukuliwa kwenye camara hivi karibuni 40 Glocc, ameendelea kuandika tweets za kumkejeli.