AY na Cpwaa kuangusha show ya ‘Road to CHOMVA 2012’ Billcanas
Wakati zikiwa zimebaki siku kama 30 tu hadi tuzo za video za muziki za Channel O zitakazotolewa November 17 nchini Afrika Kusini, wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo, Cpwaa na AY watapiga show October 28 walioipa jina la ‘Road to CHOMVA 2012.’
Show hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Billcanas wa jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 7,000.
Baadhi ya wasanii watakaowapa shavu AY na Cpwaa ni pamoja na MwanaFA na Ngwair.
AY ametajwa kuwania vipengele vitatu huku Cpwaa akitajwa kuwania kimoja.
