AY na Cpwaa kesho kukinukisha Billcanas
Wasanii wawili wa Tanzania wanaowania tuzo za Channel O 2012, AY na Cpwaa kesho watakuwa kwenye stage katika klabu ya Billcanas kwenye show waliyoipa jina la Road2CHOMVA2012.
Katika show hiyo ya kubariki uteuzi wao kwenye tuzo hizo watakuwa pamoja na wakali kama MwanaFA na Ngwair.
Show hiyo itaruka live kupitia TBC 1 na kwa mujibu wa Cpwaa crew ya Channel O nayo itakuwepo kwenye show hiyo.
Tuendelee kuwapigia kura zaidi wasanii hawa ili wailetee tuzo Tanzania.
