AskFidQ:Shyrose Bhaji avutiwa, naye ashiriki kuuliza

 

Kila weekend Fid Q amejiwekea utaratibu wa kupokea maswali kwa njia ya Twitter. Utaratibu huo ameupa jina la #AskFidQ. Mpaka sasa AskFidQ imejipatia umaarufu mkubwa kiasi cha kuwavutia hata watu maarufu na wanasiasa.

Leo hii mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhaji naye ameshiriki kumuuliza maswali kadhaa baada ya kuvutiwa na hatua ya msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda kuanzisha darasa la Hip Hop.

Haya ndio maswali aliyomuuliza.

Shyrose: Idea ya kuwa na darasa la hip hop uliipataje?

Fid: Mimi na Churchill tulikua tumekaa chini ya mwembe..ikatuijia ghafla

Shyrose: Ni kwa muda gani sasa darasa limekuwa likiendelea?"

Fid: Mwaka wa pili tangu lianze, lakini kikazi lina miezi mitatu 

Shyrose: Excellent idea,nimeskia clouds wakikupongeza,darasa lilianza na wangapi na idadi imefika ngapi?

Fid:25,Sasa 52

Shyrose: Watoto wa mtaani ni wangapi? Wapo?"

Fid: 34

Shyrose: OMG 34 its a huge # Hongera sana, Mungu atakuzidishia. Wamefaidikaje na darasa tangu kuanza kwake?

Fid: Exposure

Shyrose: Safi sana,no further Qs

Fid: Asante sana mheshimiwa.. Na pia naomba ujue tutafurahi sana ukitutembelea darasani