Anayejiita meneja wa Avril atapeli na kuteka msichana

 

Mtu mmoja anayejifanya meneja wa mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya Avril  Nyambura anadaiwa kumtapeli na kumteka msichana.

Jamaa huyo alihack akaunti ya Facebook ya Avril na kujifanya yeye ni meneja wake.

Alidai kuwa alikuwa anatafuta wasichana wa kuonekana kwenye video ya wimbo mpya wa Avril.

Mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Bolt na kupanga kukutana na msichana huyo aitwaye Claire. Mpaka leo msichana huyo hajulikani alipo.

Avril amezungumzia suala hilo kupitia mtandao mmoja wa nchini Kenya na kusema kuwa hamjui meneja huyo na kwamba alifahamu habari hizo jumatano ya wiki hii.

Msanii huyo wa label ya Ogopa DJ’s amesema ana wasiwasi mkubwa kutokana na kutojua malengo ya mtu huyo.

Polisi wanamsaka meneja huyo fake ambaye ameshaweka appointment na wasichana kibao.