
Albam yake Kanye West iko mbioni kutoka
Ni ngumu kuimagine, lakini habari ni kwamba mwaka huu mashabiki wa Kanye West watapata albam mbili kutoka kwake.
Pamoja na albam ya G.O.O.D. Music, Cruel Summer, albam ya Yeezy itatoka pia mwaka huu.
Habari hizo zilitolewa na makamu wa rais wa Def Jam, No I.D. ambaye ni mwalimu wake katika utayarishaji wa muziki.
Cruel Summer itatoka August na baada ya hapo No I.D., amesema albam yake itafuatia ambapo yeye ni miongoni mwa maproducer wa albam hiyo ya peke yake.
No.I D ameongeza kuwa yeye haproduce wimbo wowote kwenye albam ya Cruel Summer lakini atahusika zaidi kwenye albam ya peke yake Kanye.
Alipoulizwa kuhusu nini cha kutegemea kwenye albam hiyo, alisema, “This is Kanye. You know what to expect from the family. He hasn’t missed yet, so don’t expect him to miss.”