
Albam ya Top 10 ya Tusker Project Fame 5 yazinduliwa
Albam ya wasanii kumi waliongia Top 10 ya shindano la Tusker Project Fame imezinduliwa jana usiku katika hoteli ya Tribe ya jijini Nairobi, Kenya.
Albam hiyo imesimamiwa na kampuni ya East African Breweries Limited (EABL) na Universal Music Group (UMG).
Miongoni mwa washiriki wa TPF5 waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Steve, Samantha, Jackson, Nancy, Allan, Eunice, Sharon na mshindi Ruth Matete.
Wengine waliohudhuria ni pamoja na maofisa wa EABL na UMG, maceleb mbalimbali wa Kenya wakiwemo mtangazaji wa Kiss FM Shaffie Weru, Producer/Rapper Collo, mtangazaji wa KTN Ian Mugoya na wengine.
Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albam hiyo ni pamoja na wa Samantha ‘Avec wa Nancy, ‘Welede’ (This Guy) na wa Steve, ‘I’ll Be There.
Nyingine ni Sio Mapenzi wa Jackson na Ndoto Yangu wa Ruth.