
50 Cent: Kama kuna mtu anayemchukia Frank Ocean basi ni mjinga
Baada ya Jay-Z, Busta Rhymes, Beyonce na wasanii wengi wengine kumuunga mkono mwanamuziki wa kundi la Odd Future, Frank Ocean kuamua kujitangaza kuwa ni ‘gay’, 50 Cent naye ameamua kusema yake.
Akiongea na MTV UK, 50 amesema: Kama kuna mtu anayemchukia Frank Ocean basi mjinga. Nadhani Frank Ocean ni msanii mwenye kipaji, nadhani ametengeneza vitu ambavyo vilinifanya nijue jina lake, vilivyonivutia na kwa vitu alivyosema kwenye nyimbo kama 'Novacane’.
Kwake Fif, jitihada za Ocean kwenye studio zina umuhimu mkubwa kuliko anayoyafanya chumbani, na kwasababu Frank ametoa performance ya nguvu kwenye rekodi hiyo, aliyoyasema kuhusu maisha yake ya mapenzi hayana madhara yoyote kwa MC huyo wa Get Rich or Die Tryin'.
Akizungumzia kuhusu uamuzi wa Frank Ocean kuusema ukweli huo muda mfupi kabla ya kuzindua albam yake, Channel Orange, 50 amesema; "Unaweza kuuita ujasiri ama marketing,kwasababu ulikuwa ni uamuzi uloipangwa; haikuwa ajali.”