50 Cent amponda Kanye West, amwita Kim Kardashian ‘takataka’
Rapper na bosi wa G-Unit Records Curtis Jackson aka 50 Cent amemponda adui yake wa siku nyingi Kanye West kwa kuwa na uhusiano na Kim Kardashian ambaye anamwita ‘takataka’.
Akiuzungumzia wimbo mpya wa Kanye, 'Perfect Bitch', ambao amemtungia Kim, 50 Cent amedai kuwa Kim anaonekana ‘perfect’ kwenye macho ya Kanye pekee.

50 ameliambia jarida la XXL: "I mean ... if that man feel like she's perfect, then she's perfect. He could mean it and you'll end up singing the words to it because he's Kanye."
Rapper huyo aliendelea kusema kuwa uzuri auonao mwanaume mmoja unaweza ukaonekana ubaya kwa mwingine.

aliongeza: "Unajua ilivyo? Takataka ya mwanaume mmoja inaweza kuwa hazina ya mwanaume mwingine."
Rapper huyo bingwa wa kuponda amedai kuwa hajui kama kuna kitu kama ‘mwanamke aliyekamilika’.
