Tigo yawaomba radhi wateja kwa kukosekana network siku nzima, wateja watukana matusi ya nguoni

Wateja wa mtandao wa Tigo jana walijikuta katika usumbufu mkubwa baada ya mtandao huo kukata kwa zaidi ya masaa sita.

Wateja wengi wametumia ukurasa wa Facebook kutoa malalamiko yao huku wengine wakishindwa kujizuia na kuamua kutukana matusi ya nguoni.

“Habari ya asubuhi mpendwa, tunaomba radhi tena kwa tatizo la mtandao lililojitokeza, mainginia wetu wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha ili kutatua tatizo la mtandao,kwa sasa mtandao umesharudi na unafanya kazi vizuri, asanteni sana kwa uvumilivu wenu. Asubuhi njema,” waliandika Tigo kupitia Facebook.

“Ndugu wateja wetu,poleni sana kwa usumbufu mnaopata, ma enginia wetu wanajitahidi kulitatua tatizo kwa hali na mali kurudisha mawasiliano, asanteni uvumilivu.:

Haya ni miongoni mwa malalamiko ya wateja:

“tiGO you are soo F**ED UP..i will shift from this crap telecom company..and surely i will convince my friends wahame pia..MNABOA..F***K YOU TIGO..>>”

“NYIE TIGO KM JINA LENU KWELI NYIE TIGOOOOOO...MNAZNGUA LIMTANDAO LENU BOM KWELIKWELI TENA SANAAA... KAZI IMEWASHNDA SS NI KUAMIA AIRTEL+VODA+ZANTEL....KAENI NA UJINGA WENU!!!”

P****vu kabisa yan bora mngechuna et "umepata dak 2 na sms 5 kuokana na usumbuf wa jana" sa acheni up***u wenu usumbufu tulioupata hamuwez kutufidia hata cku moja xo kuwen makini.”

“Nimewachoka aiseeee, Nasema nimewakinai. Hamna maana kabisa bora nihame tu na niitahamasisha ndg jamaa na marafiki zangu wote tuhame mana mwatufanya ndondocha sasa mcxyuuuuuuuuuuuuuuu.”