Robert De Niro amchana live Jay-Z kwa kutopokea simu yake mara sita

Jay-Z anafahamika zaidi kama mfalme wa New York lakini pale anapopigiwa simu na nguli mwingine katika jiji hilo na kushindwa kuipokea kuna tatizo hapo.

Robert De Niro amempa mbovu Jay-Z kwenye sherehe ya kuzaliwa ya muigizaji Leonardo DiCaprio jijini humo.

Muigizaji huyo wa Goodfellas anadaiwa kumchana rapper huyo wa "Hard Knock Life" kwa kushindwa kupokea simu yake baada ya kumpigia mara sita ili arekodi theme song ya Tribeca Film Festival.

Shuhuda wa tukio hilo alisema, “Bob alkuwa amekaa kwenye meza pale Jay-Z alipoenda kumsalimia na De Niro kumwambia Jay kuwa hakumpigia simu baada ya kukuta missed calls."

“Bob hakuwa kwenye mood ya kufanya mazungumzo. Alimwambia Jay kuwa kama mtu akikupigia simu mara sita unatakiwa kumpigia. Haijalishi wewe ni nani. Ni ujeuri tu.”

Alisema Jay-Z alipojaribu kuingiza utani kwa kusema kuwa si mzuri katika masuala ya simu De Niro aliendelea kumwambia kuwa amemkosea heshima.

Inadaiwa kuwa baada ya kuona hali ni ngumu Beyoncé aliingilia lakini hilo halikushusha mzuka wa Robert.