Mustafa Hassanali apeleka Afrilaal Collection jijini Johannesburg

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa wa nchini Tanzania Mustafa Hassanali anatarajia kupeleka onesho la mavazi liitwalo Afrilaal nchini Afrika kusini.

Show ya Afrilaal Collection ambapo “Afri” ni kifupi cha Afrika na “Laal” likiwa ni neno la kihindi lenye maana ya rangi nyekundu itatumika kupigia debe uelewa wa HIV/AIDS.

AFRILAAL  itakuwa ni collection ya tano kwa mwaka huu na show yak eta tisa nchini Afrika Kusini.

Mustafa Hassanali, ameshawahi kuonesha mavazi yake katika nchi 16 na majiji 25 huku akitajwa kama “One of Africa’s Top Male Fashion designer  na jarida la Uingereza la NEW AFRICAN WOMAN.