Madam Rita: Usiruhusu mtu akuamulie maisha yako!

 

Rita Paulsen is the most influential celebrity in Tanzania to date! Anachokisema kinasikilizwa zaidi na kuliko mtu maarufu yeyote aliyepo kwenye showbiz Bongo. 

Kupitia Facebook jana amewapa somo mashabiki wake kuishi kwa namna wao wanavyojisikia na sio kuishi ili kuwaridhisha wengine.

”Katika haya maisha, watu watajaribu kukwambia vitu ambavyo unaweza na hauwezi kufanya. Pia watajaribu kukuamulia wewe uwe mtu wa aina fulani na mwenye tabia fulani au usiwe mtu aina fulani.

Kama kweli una uwezo wa kufanya kitu fulani na unaamini hivyo, basi usikubali kukata tamaa, ”aliandika.

Status hiyo imevutia comments 520 na likes 1,092 kutoka kwa mashabiki 14, 989 waliojiunga na page yake mpaka sasa.