Jennifer Lopez kuitosa American Idol
Mwanamuziki na mrembo Jennifer Lopez jana ameonesha dalili kubwa kuwa ataitosa American Idol kama jaji.
Katika interview aliyofanya na kipindi cha Today,JLo amesema ni muda wa kwenda sasa, alipokuwa akijibu swali la kama ataendelea kuwa jaji kwa msimu wa tatu wa shindano la kuimba la American Idol.
Jennifer, mama wa watoto wawili mapacha na mwenye miaka 42 amemuambia mtangazaji wa show hiyo Natalie Morales kuwa ulikuwa ni uamuzi mzito lakini anafikiria upya.
Anasema aliacha mambo mengine yasimame kwasababu ya kazi ya American Idol na sasa amesema anataka kufanya mambo mengine katika career yake.
Kwa sasa mrembo huyo anajipanga na ziara ya kuipromote filamu aliyoshiriki ya Ice Age 3:Continental Drift.
