Izzo B: Wasanii wanadanganya hela wanayopata kwenye show

 

Msanii wa hip hop kutoka Mbeya Emmanuel Simwinga aka Izzo B amesema wasanii wengi nchini hudanganya kiwango cha hela wanayolipwa kwenye show.

Amesema haingii akilini mwake pale anapomsikia msanii anasema amepiga show kumi ndani ya wiki kadhaa huku kila moja akilipwa zaidi ya milioni 5.

Ameongeza kuwa wasanii wengi huishi maisha tofauti kabisa na yale wanayosema wakati wakihojiwa kwenye radio.

Akiongea kwenye Spotlight ya East Africa Radio kwenye kipindi cha Power Jams leo, Izzo amesema, ‘Iweje msanii alale chini ama atembee na bajaji wakati analipwa hela yote hiyo!!”

Amesema kwake yeye pamoja na kupata simu nyingi toka kwa mapromota wanaomtaka akapigie show, huishia kupiga show tatu tu kwa mwezi kwakuwa wengi huwa na fedha kiduchu.