Diamond acheka kuandikwa kwenye mtandao maarufu duniani MSN

Mtandao maarufu duniani wa MSN umempa shavu Diamond na Lady Jaydee kwenye  kipande kifupi cha habari picha kilichopewa jina la ‘The King and Queen of Bongo Flava.’

“Bongo Flava is a genre of hip hop from Tanzania. The lyrics are in English or Swahili. Two of the biggest stars of this genre are Diamond Platnumz and Lady Jaydee,”umeandika mtandao huo jana na kuweka picha zao kadhaa.

Kutokana na kitendo hicho Diamond ameandika kupitia website yake, “Honestly nmejiskia furaha sana kuandikwa katika mtandao mkubwa kama huu,juu ya kazi yangu ya muziki ninayoifanya na kupewa heshima ya kuwa King of Bongo Flava.Hii inaonesha ni jinsi gani muziki wetu umepiga hatua na unazidi kuvuka boda.”

Hongera Diamond na Lady Jaydee.