Beyonce kuongoza na kutayarisha documentary ya maisha yake
Beyonce Knowles anatarajia kuongoza na kutayarisha documentary ya maisha yake ambayo itaonesha video za concerts zake na mahojiano ya karibu zaidi.
Mrembo huyo atazungumza mengi kuanzia enzi za Destiny's Child, albam za peke yake, ndoa yake na mume wake Jay-Z na mtoto wao wa kike Blue Ivy.
Utengenezaji wa filamu ndio field mpya anayoanza kuifanya baada ya kufanikiwa kama muimbaji wa R&B, record producer, fashion icon na muigizaji.
